Chukua muda mwingi na wanajamii walio na mgogoro na ndovu. Je, ni matukio mangapi ya mgogoro yanayofanyika na kwa muda upi?Je, ni matukio ya kila siku au ndovu huja tu katika miezi fulani? Ni migogoro ya mchana ua ni ya usiku?Ni ndovu mmoja au ni wengi? Je, ni nani ambaye jamii inatarajia awasaidie wakati wa matukio ya mgogoro?Je, kuna mgogoro uliopo kati ya jamii na idara ya wanyama wa pori Unaoongeza mfadhaiko?
Kwa kupata mara, uzito na chanzo cha mgogoro, unaweza kuanza kutambua rasilimali na kiwango cha bajeti kitakachohitajika kutatua tatizo hili. Je, kwanza ni kwa nini ndovu wanavamia shamba au mali? Je, wanatafuta chakula na maji? Je, mkulima anawavutia kwa kupanda mimea wanayopenda kula? au shamba au mali yanafunga njia asili ya uhamaji ya ndovu?
Huenda ikawezekana kupunguza mgogoro kwa kuhakikisha kuwa ndovu wana ufikiaji wazi wa chanzo cha maji, wanaweza kuingia na kutoka bila tatizo kwenye kichaka asilia ili kutafuta chakula, au kutambua na kusogeza ua unaozuia njia asilia ya uhamiaji. Usumbufu ndani ya mbuga la wanyama lililo karibu (yaani kupeleka wanyama malishoni ndani ya mbuga) pia kunaweza kuwafanya ndovu kutoka nje na kwenda kwa jamii.
Hali nyingi za migogoro husababishwa wanadamu kubadilisha shamba hivyo kwa kutambua na kuondoa mijengo au usumbufu ndani ya eneo la malisho ya ndovu, kunaweza kupunguza mgogoro kwa muda mrefu. Iambie jamii itambue kutembea kwa ndovu karibu na suala la mgogoro– yaani ikiwa ndovu wanaingia kwenye eneo la shule mwambie mwalimu achore kwenye kijikaratasi upande ambao kwa kawaida ndovu wanatumia kuingia shuleni ili kusababisha uharibifu.
Unaweza kugundua kuwa kuna sehemu moja dhaifu katika ulinzi wa mipaka inayohitaji uangalifu mkuu wa kuwekeza katika vizuizi. Usitumie rasilimali chache kwenye mipaka ambapo ndovu hawatumii kuingia. Tumia ramani kuweka rekodi ya matukio na kulinganisha kabla na baada ya tabia mara kizuizi kinapoongezeka.