Zana
Kijitabu kimegawanywa katika sehemu saba zilizoorodheshwa hapa chini.Unapofungua kila kipengele, ama unaweza kusoma nyaraka bila malipo kama kijitabu cha mtandaoni cha ISSUU, au unaweza kuingia na kusajili akaunti ili kupakua PDF shirikishi. PDF hizi zina viungo vya kupata makala za sayansi, video za nyenzo zikiwa zinatumika, na tovuti za wachangiaji wetu kwa maelezo zaidi. Utaona kwambakila nyenzo ina aikoni zilizopachikwa ndani yake. Tazama ukurasa wa Ufunguo wa Aikoni kama huelewi maana ya ishara. Kama ungependa msaada wa kuamua ni nyenzo gani utakayotazama kwanza kulingana na upendeleo wako binafsi, angalia Mwongozo wetu rahisi wa maamuzi katika sehemu ya chini ya ukurasa ambao hutoa vifurushi vya nyenzo zinazopendekezwa kulingana na tatizo lako, bajeti na muda uliopo. Bado tunashughulikia kutengeneza na kukamilisha nyaraka kadhaa, zitapakiwa kwenye ukurasa huu mara tu zitakapokuwa tayari kusambazwa. Asante kwa uvumilivu wako wakati tunafanya bidii kukamilisha mradi huu.
Iwapo ungependelea kupokea kitabu kilichosasishwa zaidi cha zana zote zilizokusanywa kama PDF kamili ya kurasa 200 (mbs 80) tafadhali nenda kwa kiungo cha pink cha “Mwongozo kamili wa HEC” hapa chini au tutumie barua pepe kwa lucy@savetheelephants.org kwa kuomba nakala.